GET /api/v0.1/hansard/entries/1283889/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1283889,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1283889/?format=api",
    "text_counter": 291,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Miraj",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Naibu wa Spika. Ninasimama kupinga Ripoti hii iliyoletwa na Kamati ya Powers and Privileges kwa sababu zangu. Kwanza, samahani kwa Karani wetu wa Bunge ambaye amepitia mengi ambayo tumekuwa tukiona kwenye ukurusa wetu wa WhatsApp . Hata mimi sipendelei jinsi anavyojibeba dada yangu, Sen. Orwoba. Jumla ya hayo, ninasimama kupinga uamuzi wa Kamati hii. Hakuna mahali popote ambapo mwanamke au mwanamume yeyote anaweza kutoa ushahidi kuwa ameombwa mapenzi. Inasikitisha kusikia katika kanda za Seneti kwamba ikiwa kila mwanamke anayeombwa mapenzi atajibeba jinsi ambavyo Sen. Orwoba amejibeba, basi tutawafunga wanaume wengi. Bw. Naibu wa Spika, kauli hio imenisikitisha sana kama kiongozi wa kike mchanga ambaye nimejitosa katika tathnia ya kisiasa. Mtakubaliana na mimi kwamba tunapitia changamoto nyingi kama wanawake na zaidi kama watoto wa kike wa umri"
}