GET /api/v0.1/hansard/entries/1283891/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1283891,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1283891/?format=api",
"text_counter": 293,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "wetu, kuweza kufikia hadhi hii ya kisiasa ambayo Sen. Gloria, mimi na wengine tumefikia. Ni jambo la kusikitisha zaidi kuona kuwa Bunge la Seneti na hata uongozi wake – Walio Wengi na Walio Wachache – wamekosa busara na hekima ya kutatua tatizo hili pindi lilipoanza. Sisi Waswahili husema, kidonda huanza kwa muwasho, kikakunwa mpaka kikakua kikubwa. Malalamishi ya Sen. Orwoba hayakuanza jana wala juzi. Nitakubaliana na Sen. (Dr.) Murango, kwamba kuna makosa mengi yamefanywa na viongozi wenza kama aliyofanya Sen. Orwoba. Kila mtu ana jinsi ya kujieleza anapokumbwa na changamoto kwenye maisha yake. Kuna watu ambao wamejitundika katika miti na ku-commit suicide kwa matatizo ambayo wangekaa na wenzao na kuyatatua. Sen. Orwoba hajafanya jambo geni ambalo viongozi wengine wa kiume hawajalifanya. Nilikuwa katika Senators Lounge wakati Sen. Sifuna alikuwa anatusi Spika wa Muda wa Bunge hili, Sen. Veronicah Maina. Alisema “ Shame! Shame!” Spika alimfurusha kwa majuma kadhaa, lakini kwa sababu ni Seneta wa kiume, siku ya pili kwa kikao cha Saa Nane, Sen. Sifuna aliregeshwa na kuendelea na shughuli zake za kuwawakilisha watu wa Nairobi."
}