GET /api/v0.1/hansard/entries/1283905/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1283905,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1283905/?format=api",
    "text_counter": 307,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Miraj",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "wamepewa vyeo kwa ajili ya kulala na wakuu katika vyama vya kisiasa. Leo, Sen. Orwoba anakuhukumiwa kwa sababu ni mtoto wa kike ambaye ametumia matumshi yasiyofaa ambayo watu hawakubaliani nayo. Nakubaliana na ndugu zangu kwamba yapo matamshi ambayo dadangu Seneta anayatumia hata dhidi yangu, lakini sisi kama viongozi tutumie hekima na busara. Tusitumie nafsi zetu kutaka kumuadhibu mtoto wa kike ambaye amepitia yale ambayo wengi kule nje wameshidwa ili kufika hapa. Sisi Nominated Senators tumeletwa kwenye Bunge kuwakilisha wanawake wengi ambao hawakupata fursa ya kufika katika nyumba kama hii. Leo nimechangia Hoja hii ili iweze kuwa katika kumbukumbu ya historia ya taifa la Kenya ya kwamba sitakubali mtoto was kike anyanyaswe kwa sababu ya jinsia yake. Uamuzi mmoja unaweza kutumiwa katika kosa hilo ambapo mwanaume ametajwa na uamuzi uwe tofauti kwa kosa lilo hilo wakati ni mwanamke. Nimetangulia kusema kwamba nasimama na Katibu wa Seneti. Yale yaliyotamkwa hata mimi nikitoka nje na mtoto wa kiume anifinyie jicho, ukiniambia nitoe ushahidi huo, sitaweza kuwa nao. Pia ni ngumu kutoa ushahidi wakati umeombwa mapenzi."
}