GET /api/v0.1/hansard/entries/1283961/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1283961,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1283961/?format=api",
"text_counter": 363,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Haiwezi kuwa mtu akipita barabarani akitabasamu, anatembea katika baraza za mji na katika majengo ya Bunge, kisha binti mmoja ambaye anadhani kwamba ni mrembo kwa wote anapomuona wakati anapita, anapiga nduru akisema anammezea mate. Ni tabia mbovu. Umenge au jinsia ya mtu haimpi ruhusa kudunisha mwingine. Yale tumeona kwenye mtandao ni kinaya sana. Seneta anaandika maneno yasiowezakusomeka na sisi ni maseneta wenye hadhi na tajriba ambayo tuko nayo hapa sasa. Nilikuwa katika vikao hivyo. Binti huyu amejipodoa sawa. Amekuja na mawakili wakiwa wamebeba majadala mazito, ila hamna chochote ndani ya majadala hayo. Ilikuwa kutisha maseneta kwamba ameleta mawakili. Wengine wetu ni walimu sio mawakili, lakini tunatumia hekima tuliyozaliwa nayo. Tulijadili tukaona kuwa huyu msichana anahitaji matibabu. Madaktari wako hapa na huo ni mtazamo wangu, Sen. (Dr.) Khalwale. Apewe dawa apone au kuna wale madaktari wa akili ambao wataketi naye wamsikize. Kama ni nyimbo, aimbiwe, kama ni maombi, bishop wako hapa wamuombee ili Jumba la Seneti likose kuwa kicheko kwa wakenya. Nimeona Maseneta wanawake hapa ambao wanasahau kwamba watahitaji wanaume siku zijazo. Lazima wavumilie. Vijana kama mimi ambao tunataka kuongeza wake lazima tuvumilie, ila nikikutazama sio kwamba nakutaka. Huenda nakuhurumia."
}