GET /api/v0.1/hansard/entries/1283969/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1283969,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1283969/?format=api",
"text_counter": 371,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Wafula",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 348,
"legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
"slug": "davis-nakitare"
},
"content": "Sitaki kupita hapo, ila naomba Maseneta tufanye kazi pamoja; tuwe na heshima. Kiongozi kama Nyegenye amechukuwa miaka mingi ya kusoma kuwa na tajriba, ana familia, hadhi na kutambulika kote ulimwenguni. Haiwezekani mtoto bado ananyonya anakuja kumpaka tope. Sisi tutasimama na mapendekezo na nadhani kwamba heshima itadumu katika Jumba la Seneti. Kwa hayo mengi, wanaume wenzangu, tukaze kamba tujitetee tunapotetea wanawake, lakini wasitumie uume wetu kama donda la kufanyia mzaha. Nikimalizia, nyinyi mnakumbuka kuna matamshi wamekuwa wakisema kama una kile kitu kitumie kikupe kile unachokitaka. Sijui ni kitu gani, shangaeni tu. Hata mimi nashangaa ni kitu gani. Lakini hicho kitu ni Katiba. Tukitumie kujilinda na kujitetea wanaume kwa wanawake, Jumba la Seneti lisonge mbele."
}