GET /api/v0.1/hansard/entries/1284155/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1284155,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1284155/?format=api",
    "text_counter": 67,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika. Tumesikia yale Waziri amezungumza kuhusu watoto ama watu wasiojiweza. Tumesikia mipango yake yote. Tunamshuru kwa yale yote amesema hapa. Tunajua alipatiwa hiyo kiti kwa sababu ilionekana atafanya kazi nzuri kwa sababu kuna wakati alikuwa Mbunge na pia tunajua atasaidia Serikali ya Kenya Kwanza. Ametueleza mipango mizuri kwa wale wasiojiweza. Katika majimbo 47, kuna majimbo madogo kama Jimbo la Embu. Kuna Mavuria, Kiambere, Muminchi, Evulori na Mwea. Huko ni pahali hakuna maji au chochote. Kuna mipango yeyote ya kufikia hawa watu ili wawaze kusajiliwa? Hii ni kwa sababu tunajua ya kwamba, wazazi wa watoto wasiojiweza wana shida nyingi na hawafaidiki na chochote. Ningependa kujua kama kuna mipango ya kuungana na gavana, chifu na viongozi wa mtaa ili hao watu waweze kufikiwa na huduma hiyo. Asante Waziri."
}