GET /api/v0.1/hansard/entries/1284187/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1284187,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1284187/?format=api",
"text_counter": 99,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika. Nimemfuatilia Waziri hapa. Amesema wanatoa vifaa ambavyo wale watoto walemavu wanahitaji na support programs kusaidia kuwalipia shule. Mimi ni mzazi wa mtoto mlemavu ambaye anasoma pale Ziwani School for the Deaf. Ni jambo la kusikitisha kwamba sisi wazazi tumeongezewa kima cha shilingi 3,500 kwa kila mwanafunzi. Hii ni kwa sababu hakuna pesa za kutosha zinazopelekwa katika shule hizi. Hata ilifikia wakati shule hizi zikaambiwa zitafungwa. Kwa hivyo, ningependa utueleze ni kima gani cha pesa huenda katika hizi shule za walemavu? Pia ni kwa nini walimu pale shuleni hukataa kupokea vifaa vya watoto ambao baadhi ya wazazi tunaweza kuwanunulia wakihofia vitaibiwa na wale wengine ambao hawana. Swali langu kati ya hili ni vifaa gani ambavyo mnawasaidia watoto walemavu kule shuleni ambavyo vinafanya wale wengine ambao tumewanunulia na fedha zetu kukataliwa kwa hofu ya kuwa vinaibiwa? Ni bayana ya kwamba hakuna vifaa ambavyo The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}