GET /api/v0.1/hansard/entries/1284285/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1284285,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1284285/?format=api",
"text_counter": 197,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kibwana",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 277,
"legal_name": "Kibwana Kivutha",
"slug": "kibwana-kivutha"
},
"content": "Asante Bw. Spika. Naomba kuchangia Hoja hii kuhusu uvutaji wa e-cigarrette ama shisha. Hili ni janga kubwa kwa vijana wetu. Wamejiingiza kwenye uvutaji wa sigara. Wanapoanza kuvuta e-cigarrette, vape na Shisha, wanajiingiza kwenye mambo mengi zaidi. Hizi sigara zimeongezewa vitu vingine kama bangi za kuwapoteza watoto wetu. Hili ni tatizo kubwa kwa afya kwani zinasababisha matatizo ya moyo, fungus kwenye kifua na pia kifua kikuu. Wanawake waja wazito, wanazaa watoto wenye kilo kidogo. Pia uvutaji unasababisha fungus ya Ngozi. Watoto wetu pia wanakuwa na addiction. Uraibu wa nicotine unasababisha vijana kutumia pombe na muguka. Ni kweli kuwa kama wazazi tumelegeza Kamba kwa ulezi wa watoto. Inafaa tuwaweke kwenye njia iliyonyooka wasiingie kwenye majaribio ya kutumia madawa ya kulevya. Tuna wanafunzi hapa leo na tunawasihi wasijiingize kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya. Kuna msemo siku hizi, “ my cigarette my choice, my shisha mychoice. Tunawaomba wasijiingize kwenye hili janga kwani ni shida kujitoa. Bw. Spika, inafaa pia tuwasaidie vijana wetu kuangalia mental health. Tunajiuliza kwa nini wanajiingiza kwenye mambo haya, na inaweza kuwa ni maswala ya mentalhealth. Ningependa kumjulisha Sen. (Dr.) Khalwale kwamba alivyosema si kweli. Alitaja kuwa wengi wa watoto wa single mothers wameingia kwenye utumiaji wa madawa."
}