GET /api/v0.1/hansard/entries/1284535/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1284535,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1284535/?format=api",
    "text_counter": 220,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13223,
        "legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
        "slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika kwa kunipa hii fursa nichangie huu Mswada; Kenyan Sign Language Bill. Huu Mswada unanuia kupeana uhai katika ibara kadhaa katika Katiba ya Kenya. Ibara ya kwanza ni ya 53 ambayo inapeana haki kwa kila Mkenya kupata elimu ya msingi na ya lazima. Ibara ya 54 inawapa Wakenya wanaoishi na ulemavu haki ya kupata elimu. Ibara ya 35 inawapa wananchi haki ya kupata habari. Kwa muda mrefu, hatujakuwa na sheria wala sera zinazoangazia jinsi viziwi wanasoma au kupata habari humu nchini. Huu Mswada unatazamia kutunga sheria ya Kenyan Sign Language ambayo itazingatia jinsi wanafunzi hawa watasoma. Wakati wa"
}