GET /api/v0.1/hansard/entries/1284538/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1284538,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1284538/?format=api",
"text_counter": 223,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Ninamshukuru Sen. (Prof.) Kamar na mwenzake, Sen. Crystal Asige, ambao wameleta Mswada huu. Nikiwa mmoja wa Maseneta katika Kamati ya Elimu, tuliona kwamba ni vyema pawe na vifaa vya kutosha na kuhakikisha hawa wanafunzi walio na ulemavu wanapata masomo bila kubaguliwa ili wakuwe na uwezo wa kushindana na wenzao ambao hawana ulemavu. Shule zinafaa kuwa na vifaa vya kutosha. Pia walimu wanafaa kuwa na mafunzo mazuri katika taasisi zetu za elimu. Pili, wazazi wa watoto wanaoishi na ulemavu huu wafunzwe hii lugha ya ishara. Mtoto anapozaliwa, anajifunza mambo mengi kupitia lugha. Iwapo mzazi haelewi hii lugha ya ishara, basi itakuwa vigumu sana kumsaidia huyo mtoto katika masomo. Tatu, jambo ambalo linaangaziwa katika Mswada huu ni kwamba lugha ya ishara inafaa itambulike kama lugha nyingine yoyote nchini. Kwa mfano Kiingereza na Kiswahili. Mswada huu unapelekea kutambuliwa kwa lugha ya ishara kama lugha ya tatu katika lugha zinazotumika nchini Kenya. Huu Mswada unasisitiza kwamba taasisi za Serikali na zisizo za Serikali ziweke mikakati ya kutosha ili wakalimani au watafsiri wa lugha ya ishara wawepo. Kwa mfano, Sen. Wambua ametaja kwamba runinga ya Citizen iko na mkalimani kwa jina Bi. Youla Nzale. Mtangazaji anaposoma habari, kuna mkalimani anayeeleza kwa lugha ya ishara maana ya ile taarifa inayotolewa kwa Kiingereza au Kiswahili."
}