GET /api/v0.1/hansard/entries/1284541/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1284541,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1284541/?format=api",
"text_counter": 226,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mwaruma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13223,
"legal_name": "Johnes Mwashushe Mwaruma",
"slug": "johnes-mwashushe-mwaruma"
},
"content": "Mswada huu unasema ni vyema mahakama zetu ziwe na watu wa kutafsiri ili kila mmoja aweze kujua nini kinachoangaziwa. Katika Bunge letu la Kitaifa na hata hili la Seneti, tunaona kuwa hakuna mwanafunzi yeyote kiziwi. Kama kungekuwa na mmoja, basi hangeelewa ninayosema. Basi ni vizuri kupitia Mswada huu, tuwe na sheria na sera za kuhakisha kuwa katika taasisi za Serikali na zisizo za Serikali, tunakuwa na wakalimani watakaokuwa wanatafsiri kwa lugha ya ishara. Tukiwa na mtu ambaye anaongea kwa lugha ya ishara, basi kuwe na mkalimani wa lugha ya ishara kwa viziwi. Mswada huu unaeleza kuwa ni vyema kuwe na msajili wa watafsiri ambaye atasajili wale wakalimani wa lugha ya ishara na Wizara ya Elimu. Wale watakaokuwa wakalimani watatakiwa kuwa na sifa fulani ambazo zitawekwa na idara ya elimu. Ningependa kukomea hapo lakini ninauunga mkono Mswada huu. Ni wakati mwafaka wa kuupitisha. Ninajiunga na wengine kuwasihi wenzangu wauunge mkono Mswada na tuupitishe. Hii ni mara ya pili ambapo huu Mswada umekuja. Ulikuja katika Bunge hili muhula uliopita na tukaupitisha. Ukaenda katika Bunge la Taifa lakini ukafilia kule. Kwa hivyo, wakati huu, tunaomba uende haraka na upite. Asante kwa hii fursa."
}