GET /api/v0.1/hansard/entries/1284551/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1284551,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1284551/?format=api",
"text_counter": 236,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bi. Spika wa Muda, neno ‘collabo’ linatumika kwenye lugha ya Kiswahili. Hivi sasa niko tayari kujibu hoja ya nidhamu ya Kiongozi wa walio Wachache kwa kuondoa neno hilo. Pengine nitapata fursa siku nyingine kulijadili neno hilo kwa kina. Mswada huu tunaoujadili ni muhimu sana. Katiba yetu imetoa haki nyingi ambazo wananchi wanastahili kupata, lakini kwa sababu ya kutokuwa na sheria za kurahisisha haki hizi imekuwa ngumu wananchi kuzipata. Moja ya zile haki ni kupata lugha ambayo itaeleweka kwa yule ambaye anazungumziwa ama anayezungumza ili mawasiliano yawe rahisi. Kumekuwa na ongozeko la matumizi ya watu wanaohitaji lugha ya ishara. Ijapokuwa wazungumzaji wa lugha za ishara wako, bado hawajafikia kiwango cha kutosha ili kila mtu afaidike. Kwa mfano, kwa muda mrefu katika Mahakama Kuu ya Mombasa, mtafsiri wa lugha ya ishara alikuwa mmoja. Aliondolewa Mahakama Kuu ya Mombasa na kupelekwa Mahakama ya Kaloleni. Alipopelekwa Kaloleni, kesi nyingi zilikwama Mahakama Kuu ya Mombasa kwa kukosa mtafsiri wa lugha ya ishara. Ikiwa Mswada huu utapitishwa na kuwa sheria utasaidia pakubwa kuongeza watu wanaozungumza lugha ya ishara ili iwe rahisi kuendeleza kazi kwa wale wanaotumia lugha hii. Jambo lingine nzuri ambalo litaletwa na Mswada huu ni kupata wazungumzaji wengi wa lugha ya ishara. Itakuwa ni rahisi kumpata mzungumzaji wa lugha ya ishara ili kutafsiri kwa wale ambao wanaelewa lugha na kusikia kama kawaida. Tunafaa tuupitishe Mswada huu. Tulikuwa tumeupitisha kwenye Bunge la tatu la Seneti lakini ukafa kwenye Bunge la Kitaifa. Safari hii ni lazima tuongeze juhudi kuhakikisha kwamba Mswada huu umepita katika Bunge la Kitaifa ili uwe sheria itakayotumika katika nchi yetu tukufu."
}