GET /api/v0.1/hansard/entries/1284579/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1284579,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1284579/?format=api",
    "text_counter": 264,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "Bi. Spika Wa Muda, nimesimama kwa Hoja ya nidhamu kuambatana na Kanuni Nambari 37 ya Bunge la Seneti kuomba kwamba Bunge lihairishe ratiba yake ili kujadili swala ambalo ni la muhimu na lina umuhimu kwa taifa, ambalo ni hali ya usalama katika Kaunti ya Lamu ambayo imesababishwa na matokeo ya hivi majuzi ya mashambulizi ya majangili Al Shabaab. Bi. Spika wa Muda, kwanza kabisa ningependa kusema kwamba japo kuwa maswala haya yanatendeka Lamu, mjadala au maelezo yangu hayahusiani kwa vyovyote na siasa za Lamu. Ni muhimu ieleweke kwamba hatuzungumzii siasa za Lamu hapa. Tunazungumzia maswala ambayo yanatendeka Lamu lakini yanaleta athari katika nchi mzima kwa jumla na hususan Kaunti ya Mombasa. Kwa muda wa kama miezi miwili hadi sasa, tumeweza kuzika askari kama kumi wa jeshi letu katika Kaunti ya Mombasa. Juma tatu zilizopita, tarehe 11tulimzika kijana The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}