GET /api/v0.1/hansard/entries/1284580/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1284580,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1284580/?format=api",
    "text_counter": 265,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "mmoja wa miaka 22. Mwingine alizikwa sehemu za Tiribe katika Kaunti ya Kwale na pia alikuwa wa umri huo huo. Kumekuwa na ongezeko la visa vya mashambulizi ya kundi la kigaidi la Al shabaab katika eneo la Lamu. Itaeleweka kwamba Kenya ilikwenda Somalia mnamo mwaka wa 2011, mwezi wa kumi ili kuzuia kundi hili la Al shabaab kuweza kufanya mashambulizi katika nchi ya Kenya. Lengo lilikuwa kuweka buffer zone kati ya mpaka wa Somalia na wa Kenya ili mashambulizi yasiweze kufanyika Kenya. Shambulizi lililokuwa limefanyika Lamu wakati huo ni kuwa mtalii mmoja aliuwawa na bibi yake kutekwa nyara na majangili hao. Ijapokuwa lengo hili la kuwapeleka wanajeshi wetu Somalia lilikuwa ni nzuri, lakini muda uliopita imeonekana kwamba sasa tumeweza kulegeza kamba na majangili hao wameweza kuingia mpaka katika Kaunti ya Lamu wanapofanya mashambulizi kadri ya wanavyotaka. Kwa sasa imekuwa karibu kila wiki kuna visa vya mashambulizi kama haya. Kuna vijiji ambavyo vimefanywa mahame katika sehemu fulani za Lamu nah hii imesababishwa na majangili hao. Mheshimiwa Spika wa Muda, ijapokuwa lengo hapo mwanzo lilikuwa ni nzuri, kwamba iweze kuleta amani katika sehemu ya kusini ya Somalia hususan mpaka wa Kenya na Somalia katika Kaunti za Garissa, Mandera na kwingineko mpaka Lamu, kwa sasa imekuwa ni taabu kwa Kaunti hizi zetu kwa sababu mashambulizi yanafanyika karibu kila wiki. Tulipata mafanikio fulani kwanza jeshi letu lilipokwenda Somalia kwa sababu liliweza kudhibithisha au kusawazisha Somalia na kukawa na usalama ili kuruhusu nchi kujijenga. Vile vile, ilisaidia kuongeza maeneo ambayo yalikuwa yanamilikiwa na Serikali ya Somalia. Sasa tunayo serikali kamili katika nchi ya Somalia. Pia tunaweza kukomboa miji kadhaa wa kadha ikiwemo Mogadishu na mji wa Kismayu ambayo ndiyo bandari kubwa ya Somalia. Katika mji wa Kismayu, kuna bandari kubwa ambayo ni kama mji mkubwa katika eneo la kusini la Somalia ambapo biashara nyingi zinafanyika. Mafanikio haya pia yameweza kuzibwa na zile hasara ambazo tumeweza kupata katika nchi hiyo. Tukiangalia, Juba valley ni sehemu inayolindwa na askari wa Kenya ambao wako katika jeshi la AMISOM yaani African Union Mission in Somalia. Eneo hilo ni kubwa na ndio headquarters ya kundi hili la kigaidi. Tumeweza kuona kwamba kila mwaka wameweza kufanya mashambulizi. Tuliweza kuona mashambulizi yaliofanyika katika Chuo Kikuu cha Garissa, watu wengi waliuliwa katika quarry na sehemu zingine. Pia tuliona vile basi zinazosafirisha abiri kwenda Garissa na kwingine vile zilishambuliwa na majadili hao. Ile kambi ya jeshi katika eneo la El Adde ilishambuliwa mwaka 2016 na karibu askari 200 wakapoteza maisha yao. Kwa hivyo, ni swala ambalo limekuwa donda sugu kwetu sisi watu wa Kenya. Pia tumeona kwamba kila siku zinapoenda, hakuna mpango wowote wa Serikali kueleza ni lini wataweza kuondoka Somalia kwa sababu Somalia sasa ni nchi kamili. Ni serikali ambayo ina jeshi na polisi wa kutosha. Hata kuna wakati waliweza kujaribu kuvunja uhusiano wa kibalozi na nchi ya Kenya. Hatuoni sababu gani sisi tusilinde mipaka yetu badala ya kwenda katika nchi ya mtu na kukaa huko ilhali tunashambuliwa The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}