GET /api/v0.1/hansard/entries/1284581/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1284581,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1284581/?format=api",
    "text_counter": 266,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13211,
        "legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
        "slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
    },
    "content": "hapa kwetu na hatuwezi kujilinda. Watu wengi wamepoteza maisha ambayo yangeweza kulindwa. Hivi majuzi, Bibi ya Mbunge wa Eneo Bunge katika Kaunti ya Lamu, alipoteza maisha na yeye mwenyewe kujeruhiwa vibaya katika shambulizi la hao majangili. Kaunti zetu, kama Kaunti ya Lamu inafanya biashara kubwa na Mombasa. Mazao mengi yanatoka Lamu kuja kuuzwa Mombasa na kuna vitu ambavyo vinatoka Mombasa na kuuzwa katika Kaunti ya Lamu. Kwa mfano, mchele, mafuta ya kupikia na vinginevyo. Mashambulizi haya yanalemaza biashara baina ya Kaunti ya Mombasa na Kaunti ya Lamu. Vile Vile, wakulima wameweza kutatizwa na mashambulizi kama haya. Kwa hivyo, kauti zetu hizo tatu zinashindwa kutekeleza mipango yake ya maendeleo kwa sababu ya mashambulizi ya mara kwa mara. Mwezi wa jana au wa nane, wanajeshi wetu katika Somalia walipambana na Al shabaab huko ndani ya Somalia na wakapoteza askari wawili. Wale askari wa Somalia hawangezikwa kule Somalia, bali waliletwa kuzikwa hapa nchini Kenya. Walizikwa siku ya Ijumaa na Waziri wa Ulinzi, Mheshimiwa Duale alihudhuria mazishi hayo yaliyofanyika hapa Kenya. Askari wa Somalia wanazikwa nchi ya Kenya ina maana kwamba kule kuna sehemu zingine kundi la Al Shabaab ndio serikali ikiwa wanaweza kuzuia watu wasizikwe kwao. Bi. Spika wa Muda, imekuwa tatizo kubwa kwa sababu tunapoteza vijana wadogo sana. Kijana wa miaka 22 aliyepata kazi mwaka uliopita, anapelekwa mstari wa mbele na anapoteza maisha yake. Labda, wazazi walikuwa wamewekeza, kwa sababu siku hizi kupata kazi ya jeshi si kwenda tu uwanjani na kuajiriwa. Ni lazima mapeni yatembee na sio chini ya laki moja, mbili au tatu. Kwa hivyo, laki tatu zinalipwa lakini baada ya mwaka mmoja, askari anapoteza maisha yake. Lazima Serikali watupe mwongozo ni lini wataondoka Somalia. Bila ya hiyo, tutaendelea kupoteza wanajeshi na vijana wetu na pia usalama utaendelea kudorora. Hii inasababisha watu kutoishi maisha yao ya kawaida katika maeneo yale. Bi. Spika wa Muda, ningeomba kukoma hapo na kusema kwamba ni muhimu Serikali itoe mwelekeo wa kuondoka nchini Somalia ili turejee kwa mipaka yetu na tuweze kulinda nchi yetu. Hatuwezi kulinda nchi yetu tukiwa nchi nyingine. Tulinde nchi yetu tukiwa ndani ya nchi yetu. Ningemwomba Seneta wa Lamu aje kuniunga mkono."
}