GET /api/v0.1/hansard/entries/1284582/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1284582,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1284582/?format=api",
"text_counter": 267,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Githuku",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13595,
"legal_name": "Kamau Joseph Githuku",
"slug": "kamau-joseph-githuku"
},
"content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa ya kuchangia Hoja hii muhimu inayohusiana na usalama katika nchi yetu na hususan kaunti yangu ya Lamu. Nashukuru Sen. Faki kwa kuleta Hoja hii ambayo inaguzia usalama wa nchi. Kama Seneta wa Lamu, kaunti iliyoathirika sana na mambo ya usalama, ningependa kutoa risala zangu za rambirambi kwa maofisa wetu wa usalama ambao usiku wa kuamkia leo, walipoteza maisha yao wakiwa katika harakati za kulinda nchi hii. Ndege waliyokuwa wakisafiria wakifanya surveillance ilipata matatizo ikiwa juu ya anga na hatimaye, hao wanajeshi wawili waliaga dunia. Hawa ni watu ninaowajua kwa sababu Jumatano iliyopita, nilisafiri na ile ndege pamoja na Wabunge wengine, tukielekea Lamu Mashariki ili kutathmini hali ilivyo ya usalama. Ni jambo la kuhuzinisha sana wakati watu na maofisa wetu wanaendelea The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}