GET /api/v0.1/hansard/entries/1284583/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1284583,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1284583/?format=api",
    "text_counter": 268,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Githuku",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13595,
        "legal_name": "Kamau Joseph Githuku",
        "slug": "kamau-joseph-githuku"
    },
    "content": "kupoteza maisha. Tuko na imani kubwa na Serikali hii na tunataka iangalie hali ilivyo ili isaidie jambo hili na kutegua kitendawili hiki. Bi. Spika wa Muda, napongeza maofisa wa usalama kwa sababu hao ni vijana wetu waliojitolea hali na mali kulinda nchi yetu. Katika mchakato wa kulinda hii nchi yetu, unapata pia wao wanaangamia. Wananchi wangu pia hawajawachwa nyuma. Mwezi uliopita, tulipoteza mama, mke wa Mwakilishi wa Wadi ya Hindi. Hilo ni jambo limehuzunisha sana kaunti yangu ya Lamu. Miezi miwili iliyopita, kuna watu walichomewa nyumba zao sehemu za Juhudi, Salama na Witho. Hao wananchi wamekuwa Internally Displaced Persons (IDPs) katika kaunti yangu ya Lamu. Hili jambo linahuzunisha sana ikizingatiwa kwamba tuko na Serikali inayofaa itulinde kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi hii. Bi. Spika wa Muda, ninatoa wito kwa Serikali iweze kulinda wananchi pamoja na mali yao. Ninaunga mkono mikakati rasmi ya kupeana suluhu ya kudumu ya kusaidia wakaazi wa Lamu. Kuna barabara Serikali imesema itatengeneza za kutenganisha wananchi na sehemu ya Boni Forest. Ninaunga hili jambo mkono pia. Serikali ifanye jambo hili la busara na kwa haraka zaidi ili tuweze kuokoa maisha ya wananchi wetu wa Jamhuri ya Kenya na pia, maofisa wetu wa usalama. Nikimalizia, ningependa Serikali inunue vyombo vya kisasa vinayoweza kujua mahali landmines ziko zinazosababisha wanajeshi wetu kupoteza maisha yao. Bi. Spika wa Muda, ninaunga mkono Hoja hii ili tuweze kuongelea jambo hili. Asante."
}