GET /api/v0.1/hansard/entries/1284589/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1284589,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1284589/?format=api",
    "text_counter": 274,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante, Bi. Spika wa Muda kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, natoa rambirambi zangu kwa wale wote waliopoteza maisha yao wakati wakifanya kazi ya kulinda nchi na kuangalia hali ya vile mipaka yetu inavyoendelea hapo juzi na jana na wakapatikana na hasara na kupoteza maisha yao katika ajali ya ndege. Pili, ninawapatia kongole wale maafisa wetu wa jeshi kwa kazi ngumu wanayoifanya. Ijapokuwa wanapitia mitihani mengi, wanaweza kuketi pale na kuona kwamba wameweza kutetea nchi yetu. Hususan pale sehemu za Kaunti ya Lamu. Kaunti ya Lamu ni mahali ambapo jamii zote za Kenya zinaishi. Panatakikawa kuangaliwa vizuri kwa sababu ni pahali ambapo panaleta uchumi mkubwa sana kwa upande wa utalii. Tumeona ya kwamba Kaunti ya Lamu imeachiliwa mbali. Sijui pengine ni kwa sababu hivi sasa Serikali iliyoingia haijali maslahi ya watu wa Kaunti ya Lamu. Visa kama hivi havikutendeka wakati wa Serikali ile nyingine. Bi. Spika wa Muda, naunga mambo ya usalama katika Kaunti ya Lamu. Kaunti ya Lamu ni mahali ambapo lazima paangaliwe kisawasawa kwa sababu imetengwa kana kwamba wako watu wengine wanaishi katika kisiwa na wengine nje ya kisiwa. Wale wanaoishi nje ya kisiwa ndio wanapata taabu zaidi hususan pande za magharibi ya Kaunti ya Lamu ambapo kuna Boni Forest. Majangili huwa wanatokea wakipiga watu ambao wameketi katika mashamba yao kwa miaka mingi na kuwaua. Imekuwa sasa hakuna mtu ambaye ana uhakika ya kwamba anaweza kulala leo na akaona kesho. Kwa hivyo, lazima Serikali izingatie mambo ya usalama kuona ya kwamba watu wa Lamu wametetewa sawasawa. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}