GET /api/v0.1/hansard/entries/1284590/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1284590,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1284590/?format=api",
    "text_counter": 275,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Badala ya kutetea watu katika maeneo kama yale, sasa hivi Serikali inagongana wenyewe kwa wenyewe. Mawaziri wanaongea tofauti. Pia, yule Economic Advisor naye anaongea vile. Sasa unashindwa, je, watachukuwa wakati gani kuangalia zile sehemu zinaendelea namna gani kwa usalama. Wakiwa kitu kimoja, wataona ya kwamba maisha ya watu wa Lamu yameweza kutetewa vilivyo. Hivi sasa, tuko katika hali ya kupigana na hali ya uchumi. Kule kwingine watu wanakufa. Watu hawana chakula na inafaa wapelekewe chakula katika maeneo ambayo yako na shida zaidi kama vile Lamu. Ni sehemu ambayo iko n a shida nyingi na inatakiwa msaada upelekwe kule. Lakini, hivi sasa chakula chenyewe hakiwezi kushuka chini. Hali ya maisha imekuwa ngumu. Kwa hivyo, watu wa Lamu wanaishi katika hali ngumu zaidi. Saa zingine, sio vizuri kuona ya kwamba maeneo fulani kama yale ya Witu yameachiliwa tu hivi. Majangili wanaweza kuingia na kupiga na kuuwa Wakenya na kwenda zao. Hatujasikia hata siku moja kuwa Serikali imeweza kushika al-Shabab mmoja wakasema kuwa huyu alikuwa akiongoza hao watu wa kuuwa Wakenya ndani ya Lamu. Serikali iaamuke; isilale. Iweze kulinda watu wake na kuona ya kwamba haki imetendeka kwa watu wa Lamu."
}