GET /api/v0.1/hansard/entries/1284628/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1284628,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1284628/?format=api",
    "text_counter": 313,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Shakilla Abdalla",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante Bi. Spika wa Muda, nimesimama kuunga mkono hii Hoja ya leo ya maswala ya security . Bi. Spika wa Muda, uchumi wetu Lamu unategemea utalii na uvuvi. Ni masikitiko sana kuona Serikali ikija kutulaumu kila leo kwa maswala ya kigaidi. Juzi, tumetishwa na Mawaziri waliokuja Lamu waliposema kwamba wavuvi wetu hawafai kwenda baharini bila vitambulisho. Kitambulisho kikipotea ni shida sana kukipata, hususan sisi watu wa Lamu tulio karibu na mipaka. Afadhali Serikali ingesema itapeana vitambulisho spesheli kwa wavuvi, ili kikipotea kinaweza kubadilishwa, kuliko kitambulisho cha kawaida kikipotea baharini. Sisi ni wachache na pale kwetu Lamu tumetengwa. Hivi sasa, tunasikitika kuona malumbano yanayoendelea Lamu baina ya viongozi. Bi. Spika wa Muda, ikiwa kuna kiongozi anajua kitu chochote, anajua njia ya kufuata na ya kupeleka ripoti ili hatua ichukuliwe. Lakini, mambo ya malumbano kwenye majukwaa yanazidisha utata, hekaheka na wasiwasi sana kwa wananchi. Tunawaomba viongozi wanaolumbana kutoka Lamu waache hayo mambo na wafanye kazi. Wamechaguliwa na wananchi kuwahudumia. Hawajachaguliwa kulumbana. Serikali ijaribu kuleta amani na kuchunga mipaka yetu kwa sababu tuko karibu na mipaka na shida ikija inatupata sisi, huku tukilaumiwa na huku tunauwawa na magaidi ila tumeishi kwa amani miaka mingi. Sisi kama viongozi wa Lamu tunataka Serikali idhibiti mipaka ya Lamu na Somalia; na ijaribu kuona kama watawandoa wale majeshi wako Somalia ili tuone kama hii shida itapungua. Bi. Spika wa Muda, hii shida imezidi tangu majeshi yetu yaende kule Somalia."
}