GET /api/v0.1/hansard/entries/1284647/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1284647,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1284647/?format=api",
"text_counter": 332,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kibwana",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 277,
"legal_name": "Kibwana Kivutha",
"slug": "kibwana-kivutha"
},
"content": "Lamu inajulikana kama mji wa tourism. Tunaomba Serikali iingilie kati ili watu wawe huru kufanya kazi zao bila uoga au tashwishi. Lakini ninaomba tu Wakenya na Serikali isilete ukabila, siasa au jambo lolote la kuvuruga zaidi. Wale wanajeshi wetu waliopelekwa Somalia warudi Kenya ili waongoze katika kutunza usalama. Tuangalie nyumbani kwanza kwa sababu mcheza kwao hutuzwa. Usalama kwanza uanze kwenu. Kama kwenu hakuna usalama, ya nini kulinda usalama katika nchi nyingine? Tunaomba Serikali ilete usalama wote Kenya kwanza, tuwe na nafasi, watu wote wawe huru kufanya kazi zao, halafu ndio tupeane usalama upande mwingine. Bi Spika wa Muda, ninatoa pole zangu na pia kuomba Serikali isaidie katika mazishi ya waliouawa. Ninaomba pia Serikali iwasaidie wajane na watoto walioachwa nyuma wasomeshwe. Asante kwa kunipa nafasi."
}