GET /api/v0.1/hansard/entries/1284764/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1284764,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1284764/?format=api",
"text_counter": 113,
"type": "speech",
"speaker_name": "Emurua Dikirr, UDA",
"speaker_title": "Hon. Johana Kipyegon",
"speaker": null,
"content": " Ahsante Bwana Spika. Hiyo ofisi ambayo Bwana Mulele anaenda kupewa ni yenye majukumu mengi sana. Kama walivyosema wenzangu, kesi nyingi nchini zimekuwa na shida. Kesi nyingi zimekaa miaka mingi mahakamani bila kusuluhishwa; aidha kwa sababu DPP hajajipatia ile nafasi ya kuzimaliza. Zaidi ya hayo, ningependa kumsihi Bwana Mulele kuwa akipata nafasi anayopendekezewa, ahakikishe kwamba amezifanya kesi zote kwa haki kulingana na yale makosa ambayo mtu amefanya. Ofisi yake isiwe ya kutumiwa na wanasiasa wala serikali kuangamiza watu wasio na hatia. Watu wengi nchini Kenya bado wako na kesi kortini licha ya kwamba hawana hatia. Ukiona mashtaka ambayo wamefunguliwa, utaona kwamba hawastahili kuwa mahakamani. Inafaa iwe kesi zimeshasikizwa na uamuzi kutolewa. Namsihi Bwana Mulele kuwa akipata nafasi hii, ahakikishe kwamba kesi ambazo hazina umuhimu wowote zisikizwe na ziamuliwe ndio nchi yetu indelee vizuri. Ahsante Bwana Spika."
}