GET /api/v0.1/hansard/entries/1285656/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1285656,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1285656/?format=api",
    "text_counter": 78,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13202,
        "legal_name": "John Kinyua Nderitu",
        "slug": "john-kinyua-nderitu-2"
    },
    "content": "Ukitembelea sehemu nyingi, unapata watu ambao wanajifanya wameenda kuburidika lakini wanavizia wengine; ni wakora. Wamebeba dawa ambayo inajulikana kwa Kingereza kama Dormicum. Wanawekea watu wakati wameenda kujiburudisha na hawana nia yoyote. Unapata mtu amewekewa dawa ambayo, kwa lugha ya mtaani inaitwa ‘mchele’ na baada ya dakika chache, wanalala na kukosa fahamu, na kuibiwa. Wengine wanakubeba na kukupeleka kwa gari na kukuibia chochote ulichonacho. Kwa hivyo, Kamati ya Usalama inaposhughulikia jambo hili, waliangalie kwa undani duka za kuuza madawa kwa sababu hapo ndipo shida huanzia. Kuna madawa ambayo imekubalika kuuzwa lakini inapaswa kuuzwa kwa mtu aliye na prescription . Unapata watu wengi ambao wameajiriwa katika maduka ya kuuza madawa hawashughuliki ni dawa ipi haipaswi kuuzwa bila prescription . Nao wakora wametafuta njia mbadala ya kuwaibia watu. Badala ya kutumia bunduki na risasi, wanatumia madawa. Ninafikiri ni vile teknolojia inaendelea kukua, watu wanaendelea kutumia njia mbadala za kuwaibia wanainchi. Ni vizuri Kamati hiyo iangazie kwa kindani na sio tu kwenda katika sehemu za burudani, lakini tuangalie pia duka za kuuza madawa."
}