GET /api/v0.1/hansard/entries/1285671/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1285671,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1285671/?format=api",
"text_counter": 93,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "Bw. Spika, ukweli ni kuwa mimi hupita mbali na mangwe kwa sababu imani yangu hainiruhusu kutumia vinyawaji hivyo. Kwa hivyo, ningependa kuondoa swala hilo kama Mhe. Madzayo hataki kuzungumzia mambo ya ‘mchele’ kuhusiana na mangwe. Ningependa kuondoa matamshi yangu. Bw. Spika, la msingi, ningependa kuchangia taarifa iliyoletwa Bungeni na Sen. Cherarkey kuhusiana na Kenya Airways (KQ). Ni kweli kwamba miaka nenda miaka rudi, KQ inapata hasara. Hasara hii inabebwa na Serikali. Inabebwa na kodi zetu. Leo ukiangalia tikiti ya kutoka jijini Nairobi kwenda Mombasa, sio chini ya Kshs15,000. Hatujui kama ni mafuta yako juu, gharama za uendeshaji wa shirika hilo ama ni madeni ambayo wanadaiwa. Vile vile, Serikali pia haijakuwa na msimamo wowote kuhusiana na shirika hili. Utapata kila mwaka ikifika wakati wa kulipa madeni, Kshs60 bilioni au Kshs50 bilioni zinakwenda. Hatujui ni mambo ngani ambayo yanafanyika. Kwa upande mwingine, Serikali hii hii inakusudia kubinafsisha baadhi ya huduma katika bandari ya Mombasa. Wametoa zabuni ya kubinafsisha berth ya kwanza hadi saba,"
}