GET /api/v0.1/hansard/entries/1285673/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1285673,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1285673/?format=api",
"text_counter": 95,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13211,
"legal_name": "Mohamed Faki Mwinyihaji",
"slug": "mohamed-faki-mwinyihaji-2"
},
"content": "na huduma nyinginezo. Kenya Ports Authority (KPA) inapeleka faidha nyingi kwa Serikali, mpaka ikatumika kama zabuni ya mkopo uliojenga Standard Gauge Railway (SGR). Kwa hivyo, tunaona kwamba Serikali hii haina msimamo mmoja kuhusiana na mashirika haya. Wakaenda kule Magharibi kwa kina Sen. (Dr.) Khalwale, na kusema hakuna ubinafsishaji wa viwanda vya sukari. Wakija Pwani, wanasema watachukua Kenya Petroleum Refineries (KPR) waiunganishe na Kenya Pipeline Company (KPC). Itakuwaje mto uunganishwe na bahari? KPR iko na mali nyingi kuliko Kenya Pipeline (KP). Hata hivyo, wanasema kwamba kwa kuwa wanataka kuboresha huduma za KPR, wataondoa KPR waiunganishe na KPC. Bw. Spika, hii Serikali haina msimamo dhabithi kuhusiana na viwanda. Kama hawana msimamo dhabithi kuhusiana na viwanda, waachane na viwanda vile vilivyo. Sisi tunajua bandari haiwezi kupata hasara daima dawama. Kwa hivyo, hatukubaliani na hili suala la kubinafsisha baadhi ya huduma katika bandari hiyo. Ndio maana ninasema ni lazima Serikali iwajibike. Kama wanaweza kulipa Kshs60 bilioni kwa KQ kwa mwaka na kuanzisha tena kazi katika KPR, haihitaji bilioni hizo. Tunajua kuna mafuta Turkana. Juzi, tuliambiwa hata wiki ijayo tutakapoenda katika vikao Kaunti ya Turkana, tutapata fursa ya kwenda kuangalia visima vya mafuta. Kusafirisha hayo mafuta mpaka Kaunti ya Mombasa ni rahisi, kuliko kusafirisha mpaka India kwenda kusafishwa. Kiwanda tuko nacho pale. Nafasi ya kuweka hayo mafuta iko ya kutosha na pia soko liko la kutosha. Kwa hivyo, ni bora Serikali irejeshe tena kazi katika kiwanda cha The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}