GET /api/v0.1/hansard/entries/1285678/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1285678,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1285678/?format=api",
    "text_counter": 100,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii. Tabia ya kuwekewa ‘mchele’ katika vilabu vya kimataifa au vya kawaida, iko. Watu wamepoteza maisha yao na wengine kuugua na hatimaye kufariki. Tunajua kuwa watu wanapoenda katika vilabu vya burudani, huwa hawana uangalifu maalumu wakati wamelewa. Ni kweli kabisa. Ninamuunga mkono kwa dhati dada yangu, Sen. Okenyuri, kwamba ni muhimu kuwe na uangalifu zaidi. Vile vile, tusisitize na tulete sheria ambazo zitawezesha kuwachunguza wauzaji wa madawa katika vituo vya afya. Siku hizi kuna mchezo ambapo mtu anaingia tu katika duka la kuuza dawa na prescription kutoka kwa Dr. Boni Khalwale, halafu unauziwa dawa. Hata kama huna prescription yoyote, bado utapata hizo dawa. Ninafikiria kungekuwa na mwamko mpya na mambo yabadilike. Madakatari na wauzaji wa madawa wachunguzwe wakati ambapo wanauza dawa. Wanapouza dawa ambazo wanajua ni za kulevya, ni lazima wachunguzwe wanauzia nani na dawa hizo zinaenda kutumika wapi kisha namna gani?"
}