GET /api/v0.1/hansard/entries/1285680/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1285680,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1285680/?format=api",
"text_counter": 102,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13585,
"legal_name": "Murango James Kamau",
"slug": "murango-james-kamau"
},
"content": "Asante Bw. Spika. Nawapa pole walio wekewa yale madawa yanayoitwa “mchele”. Kama Seneta wa Kaunti ya Kirinyaga kunakokuzwa mchele, ninawahakikishia kuwa hatuongei kuhusu hii mchele kama mchele ya kawaida kwa sababu huenda ikatuharibia biashara. Inafaa kuitwa kwa jina inayofaa; kwamba ni madawa mabovu ambayo yanayowekewa katika vilabu vingi hapa nchini na watu walio na nia mbaya. Kwanza pole sana kwao. Pili ningetaka kuunga mkono Hoja hii iliyoletwa hapa na Seneta wa Kaunti ya Nandi, Sen. Cherarkey. Jambo linalonishangaza ni kuwa shirika la ndege la Kenya Airways lina tikiti ghali kuliko ndege zingine. Ndege sio matatu, haziwezi fupisha njia zinazotumia. Hakuna anayekosa kutoa nauli. Tunalipa sote na kulazimishwa kuwa wazalendo kwa kutumia ndege zile. Hatufai kumbembeleza punda akiwa kwenye mteremko. Tumeteseka ya kutosha. Kila mtu ana ruhusa ya kufanya kazi anavyotaka ili ajipendekeze kwa wanaotumia huduma zile. Mambo haya yanafaa kuangaliwa kwa umakini. Waswahili husema ukiona manyoya, ujue imeliwa. Kuna kasoro katika shirika hili na linafaa kuangaliwa na kutatuliwa. Asante sana, Bw. Spika."
}