GET /api/v0.1/hansard/entries/1285772/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1285772,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1285772/?format=api",
    "text_counter": 194,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii. Ningependa kujiunga na Maseneta wenzangu kukubali au kutia sahihi uteuzi wa Wakili Musangi kuwa Mwenyekiti wa Benki Kuu ya nchi ya Kenya. Mimi kama Seneta wa Kaunti ya Bungoma ninatia kidole cha ndio kwa sababu Musangi ni mzaliwa wa Kaunti ya Bungoma. Vile vile mwanabondia shupavu Bw. Wanyonyi, mwanariadha Bw. Ferdinand Wanyonyi, Bw. Chebukati na watu wengi wote wazuri wanatoka Kaunti ya Bungoma. Waswahili husema chema chajiuza na kibaya chajitembeza. Wengi wamezungumza hapa sifa za Bw. Musangi na ni kweli chema chajiuza. Sitaki kumsahau Daktari Papa wa Roma Spika wa Bunge la Kitaifa ambaye pia ametoka Kaunti ya Bungoma. Jambo la muhimu ni kuwa na msingi wa sera, sheria, mikakati falsafa za kiuchumi na kuhakikisha kwamba nchi ya Kenya inarejelea hadhi yake kimataifa katika mchakato wa uchumi wa kimataifa. Sina budi kutia sahihi na kusema kwamba Mhe. Rais na Bunge limefanya jambo muhimu kumchagua kijana msomi kutoka Bungoma kuwakilisha Serikali katika Benki Kuu na kuhakikisha kwamba mchakato wa chini juu unatimizwa katika awamu ya miaka tano ya Serikali ya Kenya Kwanza. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}