GET /api/v0.1/hansard/entries/1286013/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1286013,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1286013/?format=api",
    "text_counter": 218,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": " Asante Bw. Spika. Najiunga na wewe kwa kuwashukuru ndugu zetu waheshimiwa wakiongozwa na gavana Jeremiah kwa ukarimu na makaribisho yao hapa Turkana. Nimejionea mwenyewe wakati nilipofika kwa mara ya kwanza. Kaunti zote ambazo tumeweza kwenda kwa shughuli ya Seneti Mashinani, kama kungekuwa na kupeeana zawadi ya ushindi basi, tungepea Kaunti ya Turkana. Makaribisho ya watu wa Turkana ni hali ya juu sana. Tumeyapendelea na kuyakubali. Pia tumeweza kucheza ngoma za kinyumbani za hapa Turkana na tumefurahia sana. Asante sana Bw. gavana, Waheshimiwa wenzetu na ndugu zetu wengine wote walioshiriki katika makaribisho hayo. Vile vile, ninatoa shukrani kwa ukarimu wenu na kwa kukubali tulete Seneti Mashinani hapa na tuweze kutumia Chamber yenu ambayo ndiyo Bunge lenu la hapa Turkana. Mmetupisha sisi ili tufanye shughuli. Pia, ili muweze kuwaona Maseneta ambao wengi wenu mmewaona kwa runinga. Ilikuwa sababu nzuri kuja hapa. Nyinyi pia mmetupatia nafasi kukaa hapa ili muone vile tunavyopitisha Miswada na kujibishana katika majadiliano yetu hapa ndani ya Bunge la Seneti. Ninajua kuwa tutakapoondoka, mtajifundisha mengi kutoka kwetu sisi kama ndugu zenu wakubwa tukiwa katika Bunge la Seneti. Vile vile, Bwana gavana ningependa pia kukuunga mkono katika makaribisho yako kwao. Ungewakaribisha na kuwaambia kuwa ikiwezekana, waje kule Nairobi nasi pia tuwafanyie makaribisho makubwa. Asante."
}