GET /api/v0.1/hansard/entries/1286169/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1286169,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1286169/?format=api",
"text_counter": 374,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika kwa kunipa nafasi nami nitoe maoni yangu kuhusu Mswada huu. Jambo la kwanza, tunafurahia kwa niaba ya watu wa Tana River County, ya kwamba, kumeletwa Mswada huu na kupitia kwa SenateMajority Leader . Mswada huu unaweka mamlaka mikononi mwa wale wanao simamia hospitali na zahanati mashinani. Bw. Naibu Spika, shida imekuwa ya kwamba mara nyingi katika kaunti zetu, unapata akinamama wanaenda kujifungua na hospitali zimefungwa. Hii ni kwa sababu wale casuals ambao wamejitolea kuhudumia hospitali huko mashinani hawalipwi chochote. Unapata hospitali imefungwa. Mama anaenda kujifungua hakuna hata mtu wa kufungua ule mlango. Inakuwa shida sana kwa akina mama hawa. Nilikuwa na mkutano na akina mama kutoka Milalulu Health Centre, Galole Constituency. Walituelezea shida ambazo wanapata. Sio wao pekee yao. Shida hii iko katika Kaunti ya Tana River County na kaunti zingine hapa nchini. Unapata ya kwamba, ile zahanati ambayo iko karibu na wananchi inatumikia vijiji kadhaa. Hiyo moja, unakuta hakuna wafanyikazi ambao wameandikwa na kaunti wa kutosha. Wale watu wakujitolea ndio wanafanya kazi pale. Bw. Naibu Spika, tukiwa na usimamizi wa pesa katika zahanati na hospitali hizi, itatusaidia sana kupunguza shida ya wananchi. Ninawaomba wenzangu ambao wako na tashwishwi kuhusu Mswada huu, wajaribu kuleta vipengele vya kuusaidia ili tuupitishe. Ninawaomba wanao husika kuangalia Kipengele 11 ambacho kinapendekeza kuundwa kwa county management boards na Kipengele 13 kinachotengeneza sub countymanagement board . Pia Kipengee 15 cha hospital management board . Ukiangalia hizi kamati ambazo zimetengenezwa na kazi ambazo zinafanya ni ya kusimamia zile pesa ambazo wananchi watalipa kupata huduma. Mara nyingi, unakuta ya kwamba, wale walioajiriwa katika hospitali zetu, kwa mfano, superintendent, mkubwa wa nursing na wengine, sio watu wa kutoka kijiji hicho. Kule Tana River County, unaona wafanyikazi wa hospitali wa viwango vya juu sio watu wa kutoka kwa kijiji hicho au kaunti yetu. Bw. Naibu Spika, pesa tumesema zije na ziangaliwe na wananchi wa kawaida. Lakini, daktari, superintendent na muuguzi hatoki hapo. Je, kweli tumeweka hizi pesa kwa mikono ya wananchi? Watu wanaweza kupanga mipango pale na kukosa kutumika kwa zile pesa kwa hali ambayo inafaa. Ukija kwa Kipengele 17, unaona wametengeneza health facility management"
}