GET /api/v0.1/hansard/entries/1286223/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1286223,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1286223/?format=api",
"text_counter": 428,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13586,
"legal_name": "Alexander Mundigi Munyi",
"slug": "alexander-mundigi-munyi"
},
"content": "Asante, Bw. Spika. Naunga mkono kupitishwa kwa huu Mswada kwa sababu hii pesa ni zile zinalipwa na akina mama na wazee na watoto wale hawana chochote. Inalipwa katika hospitali zetu za kaunti na majimbo zingine zile ndogo kule mashinani. Hizi pesa saa zingine zinalipwa kila mwezi halafu inaenda kwa Exchequer kwa Serikali Kuu. Naunga mkono hizi pesa ziwe zikisimamiwa na usimamizi wa hospitali zetu mashinani. Kama ni kwa mwezi mmoja, hizo pesa ziwe zikikaa kule ndio ziweze kuwasaidia watu wetu kwa sababu zikiwa zimeifadhiwa na Serikali kuu haziwezi kutolewa na kutumika kwa haraka. Pesa hizi zinaweza kuhifadhiwa na hospital kwa muda wa miezi mitano au minne. Wakati mwingine, mtu anaenda hospitali anaambiwa hakuna dawa au makaratasi ya kumwaadikia dawa. Ninaunga mkono Mswada huu kwa sababu mimi ni mmoja wa wanachama wa Committee ya Labour. Wale wafanyikazi wanaokota pesa wanakuwa na shida nyingi sana. Juzi tulikuwa na watu wa Labour wakisema wakati wa ugonjwa wa Covid-19, kuna madaktari walioiba pesa na wale wanaokota zile pesa walichukuliwa kama sio watu. Zile pesa zingekuwa pale wakati ule, zingesaidia kuwapatia kitu kidogo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard Services,Senate."
}