GET /api/v0.1/hansard/entries/1286407/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1286407,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1286407/?format=api",
"text_counter": 60,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13202,
"legal_name": "John Kinyua Nderitu",
"slug": "john-kinyua-nderitu-2"
},
"content": "Asante, Bw. Spika kwa kunipa fursa hii. Ni jambo la kuvunja moyo sana kwamba wakenya wametoka nchini kutafuta ajira kwenye nchi za ng’ambo na wanakumbwa na mashaka. Hata hivyo, Serikali ya Kenya Kwanza tayari inajaribu kuangazia mambo haya. Kwa mfano, Serikali tayari imeajiri wauguzi wa nyanjani zaidi ya 100,000. Vile vile, Serikali imepeana pembejeo ndiposa wakulima wetu wapate afueni. Kamati itakayoangazia swala hili, yafaa iiangazie kwa undani ili tupate suluhu la kudumu. Shule zetu zinapaswa kuwalinda Watoto wanaposafiri. Seneta wa Nyeri, amesoma Kauli na kuashiria kuwa kuna wanafunzi waliosafiri na kupata shida na hatimaye mmoja wao akafa. Walimu wanaposafiri na watoto wanafaa kuwaangalia ili wasipate madhara. Kamati ya Elimu ambayo inaongozwa na Sen. Joe Nyutu yafaa iangazie swala hili ili kubaini yaliyotukia; kosa lilitokea wapi? Ikiwa kosa litapatikana, Kamati ipendekeze suluhu la kudumu."
}