GET /api/v0.1/hansard/entries/1286921/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1286921,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1286921/?format=api",
    "text_counter": 146,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa nafasi hii. Ningependa kuchangia mada ya siku ya leo kuhusiana na huduma ya kimsingi katika zahanati na hospitali zetu. Naunga mkono yale mapendekezo ambayo yameletwa kwa sababu ugatuzi unaanzia mashinani na katika boma zetu. Mswada huu unaafiki kwamba katika boma karibu 100 ama watu 1,000, kuna mfanyikazi wa Serikali wa afya ambaye atahudumu na kufanyia watu kazi. Mhudumu huyu kazi yake ni kuhakikisha kwamba iwapo kuna maradhi yamechipuka katika maeneo hayo, atawasilisha ujumbe huo kwa viongozi wa taasisi husika haraka iwezekanavyo. Vile vile, kuna maradhi ya maisha ama hulka za watu ambao watu, kwa muda mwingi, hawajayagundua. Lakini wahudumu hao watapokuwa wanashughulika na pilka"
}