GET /api/v0.1/hansard/entries/1286935/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1286935,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1286935/?format=api",
    "text_counter": 160,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa sababu leo amekuwa kombamwiko katika mahakama ya jogoo na kuku. Wahudumu hawa wa afya ni uti wa mgongo wa kudhibiti maradhi na maenezi ya maradhi katika maeneo yetu ya vijiji na miji ya humu Kenya. Vile vile, jambo la muhimu ni nimeona yameorodheshwa jinsi atakavyopewa kazi na watakavyoteuliwa. Kwa sasa, wahudumu hawa hawalipwi pesa za kaunti na za kitaifa jinsi inavyotakikana. Mswada huu utakapopita, wahudumu hawa watakuwa na uhakika kwamba fedha zitawafikia popote walipo kupitia taasisi ya kiuchumi ambayo kwao, wataweza kupata nafasi ya kupokea fedha hizo. Zaidi ya hayo, ningependa wapewe nafasi kuunda ama kujihusisha na vikundi vya utetezi wa maswala ya wafanyikazi hapa Kenya. Hii ni kwa sababu tunaelekea mahali ambapo wahudumu hao wanaweza kutishwa na kuyumbishwa kwa sababu yule anaowaajiri kazi ataambiwa yenu ni kusema ndio na kama sio, uruke juu kiwango ambacho aliyekuajiri anataka."
}