GET /api/v0.1/hansard/entries/1286937/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1286937,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1286937/?format=api",
    "text_counter": 162,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Lazima tuhakikishe kwamba wanapoajiriwa, wana mbinu ya kujieleza na kujitetea na maswala yao kushughulikiwa kikamilifu katika maeneo yao ya kazi. Mswada huu unashirika watendakazi wa idara mbalimbali. Wale ambao wanahusika na maswala ya maji wako pale kwa sababu wakati wa janga la COVID-19, tuliona kwamba maji yalihusika pakubwa kudhibiti maenezi ya maradhi haya. Tumeona mhusika katika idhara ya barabara. Hao wote wanahusika kuhakikisha kwamba wananchi wanapotaka kupata huduma za matibabu, wanaweza kuzipata kwa wakati mfupi na vile vile kuhakikisha kwamba huduma hizi zinaafiki matarajio yao. Hawa wahudumu katika vijiji wanaweza kushauri wagonjwa iwapo wataenda kwa zahanati, hopitali ndogo ama hospitali ya rufaa. Haya yote yatawezekana iwapo tutapitisha Mswada huu kuhakikisha malengo yetu kama Seneti yanaafikiwa kwa sababu tutakuwa tunawamulika kurunzi na kuhakikisha wanafanya kazi kwa mujibu wa Katiba."
}