GET /api/v0.1/hansard/entries/12881/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 12881,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/12881/?format=api",
    "text_counter": 437,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Bw. Naibu Spika wa Muda, ninaomba nichukue nafasi hii kumpongeza mheshimiwa ambaye ameileta Hoja hii ya ugonjwa wa Saratani. Kama ijulikanavyo, ugonjwa huu umeathiri watu wengi sana humu nchini. Tukiendelea bila kutafuta mbinu ya kuushughulikia kikamilifu, wakenya wengi wataendelea kupatwa na madhara ya ugonjwa wa Saratani. Hivi sasa, vituo ambavyo vinachunguza ugonjwa wa Saratani kikamilifu vimebaki kama hospitali kubwa ya Kenyatta. Je, fikiria mtu ambaye hali yake ya kiuchumi ni hafifu, kama watu wa kutoka eneo ambalo ninawakilisha Bungeni la Wundanyi. Mtu akitoka Wundanyi, ajigharamie na aje mpaka Kenyatta National Hospital kuangaliwa kimatibabu kwa ugonjwa wa Sakatani ni shida. Ninaunga mkono Hoja hii kwamba, Serikali ichukue jukumu la kuhakikisha kwamba vituo vya kuchunguza ugonjwa wa Saratani vimesambazwa na kuenezwa nchini kote ili watu wapate matibabu ambayo wanahitaji. Bw. Naibu Spika wa Muda, pili, ni jambo la wazi kuwa mara nyingi ugonjwa huu wa Saratani unagunduliwa wakati umesambaa mwilini mwa binadamu kiasi hata kupata matibabu itakuwa ni shida. Ni ombi langu kuwa ugonjwa huu uweze kubainika mapema. Na utaweze kubainika mapema kama vituo vya kukagua na kupima watu ambao wanashukiwa kuwa na ugonjwa huu vitakuwa vimesabazwa nchini kote. Bila hivyo, gharama ya kutibu ugonjwa huu itaendelea kuwa juu mara wakati unapogunduliwa utakuwa umeenea mno katika mwili wa binadamu. Mwisho, tunakubaliana kuwa hali ya uchumi hivi sasa ni dhaifu kwa Wakenya wote. Watu ambao wanaweza kujimudu kifedha ndio peke yao wanapata huduma za ugonjwa wa Saratani vile inavyohitajika. Watu wengi wakienda katika hospitali zetu, wanaguzwaguzwa na madaktari wa vijijini na mwisho wanaachwa kupata maafa ambayo hawangeyapata ingekuwa hospitali inaangalia kila mtu kikamifu. Bw. Naibu Spika wa muda, ni ombi langu kwamba, Waziri anayehusika na matibabu, lile tangazo ambalo alilifanya juzi, hata akaacha Mkoa wa Pwani kabisa katika hospitali ambazo zitakuwa zinahusika na ugonjwa wa Saratani, libadilishwe na Mkoa wa Pwani upatiwe hospitali ambayo inaweza kuhusika na kuchunguza ugonjwa wa Saratani. Sioni ni sababu gani mikoa yote ipatiwe nafasi na Mkoa wa Pwani uwachwe. Kwa hayo mengi, ninaomba kuunga mkono Hoja hii."
}