GET /api/v0.1/hansard/entries/1289069/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1289069,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1289069/?format=api",
"text_counter": 72,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante, Bw. Spika. Nitajaribu kuongea kwa Kiswahili, lugha inayoeleweka. Bw. Spika, uamuzi wa muda ulitolewa, ukaja hapa na ukajadiliwa. Uamuzi huu haukuwa wako bali uliletwa hapa na Bunge la Seneti na uamuzi wenyewe ukachukuliwa kama uamuzi wa Bunge la Seneti. Maseneta wote waliokuwa hapa siku hiyo walijadiliana kama Bunge la Seneti. Hatimaye, walipiga kura na kuona ya kwamba ni sawa hatua iliyotaka kuchukuliwa, ilichukuliwe kulingana na ripoti iliyokuwa imeandikwa na Kamati ya Powers and Priviledges . Bw. Spika, uamuzi huo ulifanywa na Bunge la Seneti. Haukufanywa tena na Kamati ya Powers and Privileges, bali Bunge lenyewe. Kwa hivyo, kama kuna kitengo chochote ambacho kinaweza kugeuza uamuzi wa Bunge la Seneti, ni Seneti yenyewe. Bunge la Seneti likae na ligeuze huo uamuzi. Sio Kamati nyingine ikae mahali na igeuze uamuzi uliofanywa na Bunge la Seneti. Hisia yangu ni kwamba itakuwa vyema uamuzi wa Seneti uheshimiwe na kila mtu. Tusilivue Bunge hili heshima bali tuliweke heshima ili liheshimiwe na Wakenya wote. Kwa maoni yangu, ingekuwa bora mhusika aambiwe atoke nje ndio Bunge hili lijadili iwapo atarejea au hatarejea. Baado ya hapo, tuhakikishe uamuzi wa hili Bunge ndio umechukuliwa. Asante."
}