GET /api/v0.1/hansard/entries/128907/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 128907,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/128907/?format=api",
"text_counter": 282,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mr. Rai",
"speaker_title": "The Assistant Minister for Lands",
"speaker": {
"id": 203,
"legal_name": "Samuel Gonzi Rai",
"slug": "samuel-rai"
},
"content": " Bw. Naibu Spika, nasimama kuunga mkono Hoja hii. Ningependa kumpongeza aliye wasilisha Hoja hii na yule aliyeifanyia mabadiliko machache kwa sababu wakati umefika ambao tunafaa kujitambua na kuyajua matatizo yanayoikabili nchi hii. Tatizo la vijana kufikia wakati huu ni ukosefu wa ajira ambalo limechangiwa sana na watoto kukosa kwenda kuchukua kosi ndogo ndogo kama vile zile zinazotolewa katika vyuo vya waalimu na kusomea katika medical colleges kwa sababu ya ukosefu wa pesa. Nchi hii imekumbwa na umaskini na nilazima tukubali. Umaskini ni kilema na umefika wakati ambapo tunapoona Hoja kama hii, ni jukumu letu kama watunga sheria kuangalia ni njia gani mwafaka inayoweza kutumika ili kuokoa vijana hawa ambao kwa muda mrefu wamekuwa mara kwa mara wakiitwa katika medical colleges na vyuo vya waalimu lakini hawawezi kwenda kwa sababu ya ukosefu wa pesa. Kwa kuwahusisha katika mpango huu wa mkopo, watoto hawa watasaidika ipasavyo. Nina imani ya kwamba jambo hili litapunguza idadi ya vijana ambao mara nyingi hawabahatiki kuwa na masomo kama haya. Ni maombi yangu kwamba tunapoendelea kufanya mambo kama haya ama kuhamasisha sheria ya bodi ya mikopo--- Serikali ilitoa elimu bila malipo. Kumekuwa na ongezeko la watoto wanaomaliza masomo. Ili kuongeza na kuokoa vijana hawa ambao ni taifa la baadaye, nadhani umefika wakati ambapo hata vyuo vya ufundi vitawajibika kutoa masomo yasiyo na malipo kwasababu kama watoto hawa wote wangepata taaluma yao katika vyuo vya ufundi, naamini matatizo mengi ya ukosefu wa ajira yangepungua na watoto wengi hawangebaki manyumbani kwasababu ya hali hii ya umaskini ambayo imekita katika nchi yetu. Ningetaka kumuunga mkono Bw. Imanyara kwa kusema kwamba ofisi za bodi ya mikopo zafaa kupelekwa katika wilaya kule tunakotoka. Tatizo moja kati ya matatizo yanayokumba watoto wetu ni kwamba wanapopewa fomu hizi na kuziwasilisha Nairobi, jambo hili huwa kama mgonjwa anayeenda hospitalini na kuandikiwa dawa na badala ya kupewa dawa hizo, anaambiwa aende anunue dawa. Mgonjwa huyo analazimika kwenda nyumbani bila dawa. Ni lazima tupate njia ya kuyaangalia mambo haya ili tuwasaidie vijana wetu. Ni lazima tuseme ya kwamba CDF imejaribu kusaidia katika mambo mengi. Asilimia 50 ya pesa za CDF huenda kwa mipango ya elimu lakini hazitoshi. Tumekuwa"
}