GET /api/v0.1/hansard/entries/128909/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 128909,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/128909/?format=api",
"text_counter": 284,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "tukilia hapa kwamba pesa hizo zinafaa kuongezwa kuwa asilimia 5 ya Bajeti. Kule nje kwa sababu ya kutoeleweka, inaonekana kwamba hata Wabunge kusimamia pesa ya CDF limezoa utata. Pesa nyingi zimepotea. Ukiangalia pesa zile ambazo zimepotea katika Goldenberg na Anglo Leasing, kama zingalikuwa zimepewa HELB, naamini kwamba watoto wengi wangekuwa wamepata masomo ya kutosha na wangekuwa wamesaidika. Ninamshukuru aliyeileta Hoja hii kwa sababu Bodi inayohusika inafaa kuandika mapendekezo ambayo yatasaidia nchi hii ili Wizara ya Fedha iwaongeze pesa na hata kile kiwango wanachopata sasa hivi kiongezwe. Kuna haja gani ya mtoto anayefanya utafiti na mambo mengine kupewa Kshs35,000 peke yake? Ikiwa pesa hizo zinaweza kuongezwa, itakuwa jambo la kusaidia. Bw. Naibu Spika, ni lazima tuseme ukweli. Ingawa bodi hii inafanya kazi nzuri, kuna uhaba wa pesa. Wakati haujapotea kwa sababu bodi hii ina muda wa kutayarisha mapendekezo yake na kuyawasilisha kwa Ofisi ya Naibu wa Waziri Mkuu na Wizara ya Fedha ili waongezwe pesa wakati wa Supplementary Estimates. Kuna parallel programme ambayo pia imehusishwa katika mipango hii. Kuna baadhi ya watoto ambao wanapelekwa nje kusoma. Kabla ya vibali vya watoto wetu kuenda nje kupata masomo vitolewe, kuna haja ya Serikali kuweka sheria mwafaka ya kujaribu kulinda watoto wanaoenda nje. Kwanza, tunafaa kuhakikisha kwamba wanaopeleka watoto nje wana uwezo huo. Watoto wengi huenda kusoma katika nchi za nje na wanapofika huko, wanaanza kufanya kazi ambazo si haki kwa binadamu kwa sababu ya ukosefu wa pesa. Pengine akiagiza pesa kutoka nyumbani, pesa hazipatikani. Kwa hivyo, ni lazima ajihusishe na mambo ambayo si mazuri kwake yeye mwenyewe na pia kwa nchi hii. Kuna haja ya kuwa na sheria mwafaka ambayo itawalinda watoto hawa kabla hawajapata vibali vya kutoka nje ili kuhakikisha dhahiri kwamba kuna pesa za kutosha za kuhimili watoto hao mpaka wamalize masomo yao wakiwa nje. Haki za watoto ni lazima zilindwe. Tumesema mara nyingi kwamba hata watoto ambao wanaokwenda katika mfumo wa parallel programme, hata kama watapata pesa za HELB, ni lazima tujiangalie kama tumejitayarisha. Kuna haja gani ya kufanya kosi mwaka mmoja halafu mwaka wa pili hauwezi kuendelea kwa sababu mambo yameharibika? Huwezi kurudishiwa karo ambayo umelipa kwa mwaka wa kwanza. Kwa hivyo, itakuwa vigumu kwa mwanafunzi huyo kulipa mkopo huo ili tuweze kuwasaidia watoto wengine. Kuna haja ya kuwa na sheria ambazo zitatusaidia kuokoa hali hii. Uhuru umepatikana lakini jambo moja ambalo Serikali lazima ipambane nalo ni kuhakikisha kwamba imepambana na tatizo la kutokujua kusoma na kuandika. Watoto wengi hawamalizi masomo yao kwa sababu ya ukosefu tulionao. Ni lazima niipongeze Serikali kwa kukubali kwamba watoto wanaotoka katika shule zetu za misingi wanafaa kupewa chakula hata wakati wa likizo ili waweze kuendelea na masomo na kuhakikisha kwamba masomo yao hayakatizwo. Jambo la kusikitisha ni kwamba kufikia wakati huu watoto katika sehemu nyingi kame wameanza kuacha shule kwa sababu ya ukosefu wa chakula. Ninajua Serikali ilizindua msimu wa kusema ingesambaza chakula kwa kutumia magari ya kijeshi lakini magari hayo hayajarudi tangu yalipotoka. Chakula kimo katika maghala na watoto hawawezi kupata chakula. Hii ni hali ngumu."
}