GET /api/v0.1/hansard/entries/1289123/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1289123,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1289123/?format=api",
"text_counter": 126,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": "Bw. Spika, katika malalamishi haya, ninazingatia ya kwamba hawa wamekuwa wakizaana. Nambari yao imeongezeka. Hili shamba lililoko hapa Pumwani ni haki yao kupewa. Hivi sasa tunaona hiyo shamba imeanza kugeuzwa. Wale matajiri wamefika hapo sasa. Mipangilio imefanywa na imepelekwa katika hii Serikali ya Kaunti ya Jiji la Nairobi. Wametolewa katika ile ardhi yao waliokuwa wakiishi pale na wanafurushwa watu wengine wanapewa. Sisi tunasema ya kwamba malalamishi haya yalioletwa ni ya muhimu sana. Ile Kamati ambayo itahusika na kuangalia hii ardhilhali iangalie kwa uangalifu sana kuona kwamba wale watu wa Pumwani wamepewa haki yao kama Wakenya wanaoishi katika nchi hii na kama haki wanayohitaji wafanyiwe na serikali yao."
}