GET /api/v0.1/hansard/entries/128913/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 128913,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/128913/?format=api",
    "text_counter": 288,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Hivi sasa, kuna baadhi ya watoto ambao wameitwa katika vyuo vya mafunzo ya walimu na utabibu. Watoto hao wanahitaji msaada kutoka wa Wabunge. Kitengo cha CDF hakijapata pesa kwa sababu mwaka ulifungwa na hakuna pesa. Watoto hao wanahitaji kwenda shuleni na hatuna njia ya kuwasaidia. Kwa hivyo, ikiwa msimu huu unaweza kukamilishwa kwa wakati unaofaa, nina imani tunaweza kuwaokoa watoto hao ambao tayari wametishika kwamba hawataweza kuchukua nafasi zile. Utafika wakati kwamba mwenye nguvu pekee ndiye atakayeweza kuwapeleka watoto wake shuleni. Lakini, mnyonge, siku zote, ataendelea kubaki nyuma. Haikuwa nadhiri ya Serikali hii kwamba wakati wote ni wenye nguvu ndio watafaidika na wanyonge wataendelea kuumia. Kwa hivyo, Hoja hii ikipitishwa, watoto ambao tayari wametishika kwamba hawataingia katika vyuo tofauti tofauti wataweza kuendelea na masomo yao. Kama itawezekena pia, hata zile taasisi ambazo zimewaita watoto hawa, zinafaa kuwa na mawasiliano ya kutosha ili kuhakikishe kwamba, wakati mipango inapoendelea kutengenezwa, watoto hao watakubaliwa kuingia katika vyuo vyao. Kwa sababu, utafika wakati ambao wataambiwa kuwa nafasi zimefungwa ili wenye nguvu, ambao wako tayari hata kuhongana wachukue nafasi zile; watafanya hivyo na wanyonge watabaki nyuma. Tukitaka kuwaokoa wanyonge, ni lazima tutoe mapendekezo fulani ama taarifa fulani kwa hizo taasisi ili zipate kujua kwamba watoto hao wanahitajika kuchukua nafasi zile, ili nao pia wapate nafasi ya kujiendeleza kimasomo. Najua tuna matatizo mengi. Lakini swala la elimu ni muhimu katika taifa. Iko haja ya kuhakikisha kwamba mambo haya yametiliwa maanani ili tuokoe nchi yetu ipasavyo. Kwa hayo machache, naomba kuunga mkono."
}