GET /api/v0.1/hansard/entries/1289204/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1289204,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1289204/?format=api",
    "text_counter": 207,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 348,
        "legal_name": "Davis Wafula Nakitare",
        "slug": "davis-nakitare"
    },
    "content": "Asante sana, Bi. Spika wa Muda kwa nafasi hii. Kamati ya masuala ya Shakahola ilijadili kwa mapana na marefu, wahusika wakuu katika mchakato wa kupambanua na kupata ukweli wa mambo yanayoendelea Shakahola hawakupewa nafasi ya kujieleza ili kuhakikisha kwamba ripoti itakayoletwa katika Seneti hii ni kamilifu. Unafahamu kwamba matokeo ya Kamati hii itapeana mwelekeo mwafaka katika masuala ya dini na itikadi za kidini katika nchi ya Kenya. Yote ambayo tutaleta hapa itakuwa kumbukumbu ya kazi ambayo Maseneta walipewa kuhakikisha kwamba mambo ya kidini na kiroho yanaweza kudhibitiwa katika muktadha wa maendeleo. Kamati imeomba muda mwafaka ili wahusika wajieleze kisha tutamatishe na kuleta ripoti ili Serikali iweze kutekeleza mapendekezo ambayo tutakuwa tumeleta. Kwa hayo, ningependa kuunga mkono yale ambayo mwenyekiti wa Kamati amesema. Tunaomba nafasi kukamilisha yale ambayo tulipewa kufanya."
}