GET /api/v0.1/hansard/entries/1289211/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1289211,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1289211/?format=api",
"text_counter": 214,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": {
"id": 679,
"legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
"slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
},
"content": " Asante, Bi. Spika wa Muda. Kwanza, Kamati hii inayochunguza maafa yaliyotokea na miili kupatikana inayopita 95 na Zaidi; hivi sasa idadi ni zaidi ya 500. Tukizingatia kwamba watu walipoteza maisha yao, ingekuwa vyema tupate ripoti nzuri. Ripoti hii inaweza patikana kulingana na muda ambao wanakamati wanahitaji, ikiwa wameomba muda uongezwe, ili waweze kukamilisha na kuwaambia Wakenya yaliyojili kulingana na ule uchunguzi waliofanya, basi litakuwa jambo nzuri kuongeza. Hili ni jambo la kusikitisha. Watu wa Kilifi wanasikitika na wana majonzi mengi kwa sababu ni kwenye ardhi yao ambapo kila uchao watu wanafukua miili. Hata ikiwa hatuhusiani kidamu, hawa ni Wakenya kama sisi. Ni jambo la kusikitisha kwa familia kupoteza jamii zao. Mwenyekiti wa Kamati, Sen. Mungatana ametoka kwenye maeneo ya pwani na ningependelea kuona ripoti nzuri. Kamati ipewe wiki mbili kukamilisha kazi inavyo wafaa. Asante, Bi. Spika wa muda."
}