GET /api/v0.1/hansard/entries/1291509/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1291509,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1291509/?format=api",
    "text_counter": 152,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13585,
        "legal_name": "Murango James Kamau",
        "slug": "murango-james-kamau"
    },
    "content": "Bw. Spika, kuna wale wanaratibu mgao unaopewa makaunti kwa sababu ya madini au zile bidhaa zinazotokana na mahali pale. Tungependa kujua kama ni hii Kshs100 iliyopewa Kirinyaga na imetokana na madini gani? Kwa sababu, hili jarida niko nalo ni ghali kuliko Kshs100. Haina haja ya kuratibu Kshs100 za kupea Kaunti nzima. Ninaamini kuna hesabu inapaswa kuangaliwa kama iko sawa. Kama mkaazi wa Kirinyaga, ninajua eneo lililo chini ya Mwea ni muhimu kwa uchimbaji wa kokoto na marigafu mengi ya kutengeneza barabara. Kwa hivyo, kupata Kshs100 imeleta mshtuko kidogo. Bw. Spika, ninaunga mkono mambo kama haya yanaletwa katika Bunge la Seneti. Wakati tunafika kugawana pesa, kama zile za maktaba, kila wakati utapata Kirinyaga haipewi kwa sababu hatuna maktaba. Nikiulizia, ninaambiwa pesa zinagawanywa kwa wale ambao wana maktaba. Lakini, tukienda kugawa zile pesa za zile kaunti zilizoachwa nyuma, zinapewa wale ambao hawana vitu tulivyo navyo. Ni lazima tuchukue msingi mmoja. Kama watu hawana, wapewe na kama wako nayo, pia wapewe. Tunaona pia kwa mambo ya mahabara, tunabaguliwa kwa sababu hadi wakati huu, sisi tuko baadhi ya kaunti 23 ambazo hazina mahabara. Hili ni jambo nitaenda kuangalia. Asante, Bw. Spika."
}