GET /api/v0.1/hansard/entries/1291514/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1291514,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1291514/?format=api",
"text_counter": 157,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika, kupatia Embu Kshs2,142 za madini ni kama kutukana Kaunti ya Embu. Saa hiyo tunajua ya kwamba stima inatoka Embu, ikipelekwa pande zote za nchi lakini ile pesa tunaweza pewa juu ya stima ni kidogo sana. Ni sawa tumeongezewa Kshs100 milioni, lakini pia ni vizuri wale wanagawa pesa wawe wakiangalia kitu kama kura-moja, shilingi-moja. Tumeona sasa Kaunti ya Embu itakua na Kshs6 bilioni, lakini tuna mahitaji ya elimu, kilimo, afya na mambo mengi na hizi pesa hazitoshi. Utaona kaunti zingine zimepewa Kshs15 bilioni, lakini ukitembea pale baada ya miaka tano, utaona ni kama pesa imeporwa. Wengine watakua na Kshs200 bilioni na hakuna kitu watakua wamefanya. Ule wakati mwingine ujao, nitaunga kura-moja, shilingi-moja. Asante, Bw. Spika."
}