GET /api/v0.1/hansard/entries/1291660/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1291660,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1291660/?format=api",
    "text_counter": 303,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "mtoto wake. Tulipofika hapo, tofauti ya miaka ile nilikua Eldoret na wakati huu wa mwisho nilipoenda, ni kama mbingu na nchi. Niliona barabara nzuri na watu wazuri kutoka pale uwanja wa ndege. Wakati huo zamani, kulikua hakuna uwanja wa ndege, lakini wakati huu, niliona uwanja wa ndege mkubwa na mzuri. Nikaona pia jiji safi. Tulipokua tunatoka huo uwanja kwenda hotelini, hatukuona takataka kwa barabara zikiwa zimwemwagika ovyo. Nilifurahia mandhari ya Eldoret na zile siku tulikaa huko. Leo hii nikiitwa kama Seneta kupitisha ombi lao la kuwekwa cheti cha jiji kuu, nitasema niko pamoja na wao. Ninapea pia, hongera Kamati ya Ugatuzi kwa kazi ambayo wamefanya kutembea kule, kujua hali zao, kuwauliza maswali na kutoa hii ripoti iliyo mbele yetu kuijadili. Bw. Naibu wa Spika, kama Seneta wa Tana River, ningependa wale walioshikilia ugavana pale Tana River waangalie vile wenzetu wanafanya nje ya Kaunti yetu. Hapa tumeambiwa kwamba usafi wa jiji ni kitu muhimu katika kuangalia kama jiji litaitwa mji mkuu au city . Saa hii kule Tana River, ukitoka sehemu za Bangale ukielekea Garissa, unaona uchafu wa makaratasi ya plastiki. Gavana yuko lakini hakuna usafi unaotekelezwa katika majiji yetu. Sio Bangale peke yake. Nenda Garsen, Hola na kila sehemu. Ni kama nchi haina kiongozi na yeye yuko pale tu. Tunataka watu waangalie vile wenzao wanafanya, mpaka wanakuja kutoka manisipaliti wanakua jiji kuu. Ni lazima tujifunze kutoka kwa wenzetu. Bw. Naibu Spika, hapa kati ya mambo ambayo yanatikikana ni kua na chumba cha kufadhili maiti. Gavana wa Tana River, ambaye anakaa Muhula wa pili, hajawai kuona umuhimu wa kutengeneza mahali pa kuweka maiti zetu. Huyu ni Gavana mzima anatumikia Muhula wa pili! Watu wanaingia gharama kubwa sana kuleTana River. Hii jumamosi tunaenda kuzika mwalimu. Huyu mwalimu aligongwa na bibi yake akapata mshtuko. Baada ya siku tatu, huyo bibi akafa, lakini huezi kuweka maiti Garsen, Hola au Bura. Ni mpaka uende kaunti ingine. Hii ni aibu kubwa sana tuko nayo bwana! Tukizisema hapa, tunasikia vibaya na tuko na Gavana ambaye anapata pesa. Nikipitisha pesa hapa pamoja na wenzangu, anaenda kule na badala ya kupanga mambo ya maana, tunasikia mambo hata hayako katika hii Kenya. Huyo ndio Gavana tuko naye saa hii. Bw. Naibu Spika, tukiangalia health facilities zilizoandikwa hapa, Eldoret wametengeneza mambo yao na yakasimama vizuri na ndio maana leo, wamekuja kifua mbele wakisema wanataka kupewa nafasi waitwe jiji kuu. Vituo vya afya kwetu havina madawa na tuko na Gavana, yuko tu pale. Kama ule mwalimu alikufa juzi aligongwa na basi, unafika kwa kituo cha afya kilicho karibu, unapata watu wa kukuhudumia hawako na mtu anakufia pale ukimwangalia. Na saa hio tuko na serikali ya Kaunti. Imekua aibu mpaka watu wetu wakitoka Tana River kwenda kaunti zingine kufanyiwa matibabu wanakataliwa. Wanaambiwa kila kaunti inapata pesa za ugatuzi kwa hivyo, waende wakatibiwe kwao. Hivyo ndio hali ilivyo. Bw. Naibu Spika, tunasema magavana wengine na sio wa Tana River peke yake, waangalie mfano wa Eldoret na vile mambo yanapangwa ili nchi iendelee. Hapa Sen. M."
}