GET /api/v0.1/hansard/entries/1291662/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1291662,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1291662/?format=api",
"text_counter": 305,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Mungatana, MGH",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kajwang’ amesema anataka kuwe na mijiji mikubwa 47 humu nchini. Lakini, je magavana wako macho na kuangalia vile wenzao wanafanya? Kuna watu wametafuta hizi nafasi ili wajitajirishe wenyewe. Hawana mioyo ya kusaidia wananchi na Mungu anawaona na siku zao zitafika. Sio kupoteza kiti peke yake. Ni lazima wasimame wakati wataulizwa vile walipewa nafasi ya kua Gavana wa jimbo au gatuzi fulani, walifanyiwa nini watu wao. Bw. Naibu Spika, tunaomba sana magavana waige mfano wa hii Kaunti ya Uasin Gishu vile wamekuja kufanya kazi zao mpaka Kamati ya Ugatuzi ikaenda kukagua na ikapitisha. Kaunti ya Uasin Gishu walikua kifua mbele kwamba mambo yao yatakua sawa na kweli Kamati hii imeleta ripoti tuliyoifurahia. Nilifurahi nilipoenda Eldoret katika usafiri wangu wa mwisho. Tuliona tofauti kati ya Eldoret tuliyoijua na Eldoret ya sasa. Kwa hivyo, nawaomba wenzangu tulio na Hoja hii leo tuipitishe bila kupoteza wakati. Asante, Bw. Naibu wa Spika na Mungu akubariki."
}