GET /api/v0.1/hansard/entries/1291685/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1291685,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1291685/?format=api",
    "text_counter": 328,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Naibu Spika, kutoka Mungu aumbe mbingu na nchi mpaka tupate uhuru, katika Kaunti ya Turkana kumekuwa na vita juu ya mifugo na pia janga la njaa. Pia kumekuwa na shida ya vita kati ya watu wa Turkana, Uganda, Ethiopia na majirani wao wa Pokot. Kutoka tupate uhuru mpaka mwaka wa 2013, Turkana imezidi kuwa na shida hiyo. Kutoka wakati huo wa mwaka wa 2013 mpaka miaka kumi, Turkana imekuwa na shida ambayo haijaisha. Cha ajabu, nashukuru Mungu kwa sababu ya watu wale waliosema kuwe na ugatuzi. Katika nchi ya Kenya tuko na kaunti 47. Katika kaunti hizo 47 inasemekana kuwe na idara kumi na zimekuwa zikipata pesa. Kaunti ya Turkana kwa miaka 10 imekuwa ikipata karibu pesa taslimu Kshs1.3 bilioni. Kwa mwaka imekuwa ikipata karibu Kshs13 milioni. Wakati huo, Embu Kaunti imekuwa ikipata karibu Kshs6 milioni. Jambo la ajabu ni kuwa wale waliotengeneza hii sheria, ilikuwa ni kwa ajili ya kuwaunganisha wale watu waliojuu na wale walioko chini na hawajiwezi, iliwaweze kupata pesa ya kujimudu kimaisha na maisha yao yaweze kwenda vizuri. Kutoka wakati huo mpaka leo, ile kaunti ya Turkana imekuwa na shida. Kwa mfano, kumekuwa na mambo ya janga la njaa na vita. Unapata kwamba hakuna hata mti moja. Utakuta kuna shida hadi vitu vilivyotengenezwa na serikali za awali wa zamani vyote vimezoroteka."
}