GET /api/v0.1/hansard/entries/1291689/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1291689,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1291689/?format=api",
    "text_counter": 332,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "watu wanaoitwa Auditor-General, pesa taslimu Kshs100 bilioni ama Kshs130 bilioni tunataka kujua ziko wapi. La pili, mimi nikiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Ufugaji na Uvuvi, tulitoka Turkana Town tukaenda pahali ambapo mambo ya kilimo yanafanywa. Tulikuta kuna irrigation . Wale tulifikiria tutakuta watu wanalima wengi ama serikali inalima, tulipata ekari 10 pekee ambayo inalimwa na mama mmoja na bwana yake. Jambo la huzuni ambalo alituambia ni mambo ya vita. Tulisikia hata mambo ya mbolea na mambo ya National Cereal Produce Board (NCPB) hawajui. Juzi nilisikia wakisema kuwa hatukuwapa muda wa kuongea. Sisi tuliwapa muda wa kuongea lakini mambo ambayo walisema ni mambo ya vita. Jambo la ajabu ni kuwa utakuta kuwa hakuna jambo nzuri linaloendelea kule. Kwa hivyo, hadi sasa Seneti ikitaka kusaidia ili mambo ya ugatuzi isiishe, ni mradi tuwe macho. Tuliangalia ile shamba na la kushutua, yule mama alikuwa analima heka10 na zile zingine haziwezi kulimwa. Kwa hivyo, kama vita havingekuwapo, yale mambo yangekuwa yanaendelea vizuri. Siku ya pili tulienda mahali pa uvuvi wa samaki. Tulipata kampuni moja ambayo ilijengwa miaka mingi ambayo imezoroteka. Tunataka kujua zile pesa zinazopelekwa Turkana zinafanya kazi gani kwa kuwa hakuna kitu chochote kinachoendelea pale. Watu wa Turkana wako na shida na msukosuko wa vita. Hata wakati magari yanaendeshwa kwa njia, unakuta jua ni kali sana na kila mtu anaomba maji. Jameni kwa sababu hii Upper House, kutoka sasa, mfikirie vile mtaokoa baadhi ya kaunti. Hii ni kwa sababu kaunti nyingi ziko na pesa nyingi lakini hazijafanya kazi inayofaa. Mwisho ni mambo ya uvuvi wa samaki. Ile kampuni imezoroteka. Samaki walio pale kama wanaweza kuangaliwa vizuri na pia kilimo, wale watu watapata chakula. Kwa hivyo naomba serikali na Seneti tuungane pamoja tuweze kuona vile tutasaidia wale watu wa Turkana na Kaunti zile zingine zilizo na shida. Nikimalizia, Seneti inastahili iseme kuwa kama kuna Kaunti 47 na ziko na kazi nyingi, ningependa kusema pengine kuwe na kila Kamati itakayosimamia kama Kaunti 10. Kwa njia hiyo, kwa Kipindi ya miaka mitano tunaweza kuona vile tutaweza kusaidia wale watu wa Turkana. Naomba Sen. Oketch Gicheru, asimame aniunge mkono."
}