GET /api/v0.1/hansard/entries/1291712/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1291712,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1291712/?format=api",
    "text_counter": 355,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Murgor",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante sana, Bw. Spika wa Muda. Nashukuru kwa kunipa nafasi. Ninakubaliana nawe kuwa ni lazima tujichunge ili tusiwe wachochezi katika unenaji wetu. Singependelea jina la Mhe. Rais litajwe kwa sababu ya yale yanayojili kule Sondu. Kuna sehemu nyingi ambazo shida kama hii inaendelea na haihusu Mhe. Rais kwa njia yoyote ile. North Rift ambapo mimi, Mhe. Rais na viongozi wengi wanatoka, kuna shida hii. Lazima tuangalie shida iliyopo kisha tuitatue. Pia singependelea twende Turkana Kaunti na kuafikia kuwa Wapokot ni wabaya kwa sababu wameua Waturkana. Tangu mwanzo wa mwaka huu Wapokot zaidi ya 30 wameuwawa. Hatusemi kuwa Waturkana ni wabaya, ila uovu unaoendelea ni mbaya. Wale wanaoua Waturkana ni watu wabaya. Hatufai kuelekeza kidole cha lawama kwa jamii moja. Jamii hizi zimekuwa na hali hii kwa miaka mingi kwa sababu ya tabia zilizoko. Tabia hizi zinaletwa na ukosefu wa maji na upungufu wa chakula. Haitasuluhisha kufikiria kuwa Sondu Wakipsigis ni wabaya na Wajaluo ni wazuri. Tutafute suluhu ili tuweze kuleta watu wanaozozana katika sehemu tofauti pamoja. Viongozi wakichochea kikundi kimoja dhidi ya wengine, itakuwa kama kumwaga petroli juu ya moto."
}